Tanzania yatumia Siku ya Umoja wa Afrika kutangaza utamaduni wake

LILONGWE- Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi umeshiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Afrika yaliyofanyika jijini Lilongwe tarehe 9 Septemba, 2023.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola (mwenye nguo yenye nakshi za bendera ya Tanzania) akimshuhudia Waziri wa Viwanda na Biashara wa Malawi, Mhe. Simplex Chithyola akionja chakula cha kitanzania wakati wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Afrika yaliyofanyika jijini Lilongwe tarehe 09 Septemba 2023. Ubalozi wa Tanzania umeshiriki maadhimisho hayo kwa kutangaza fursa za uwekezaji, utalii kupitia Filamu ya The Royal Tour na kuhamasisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili.

Katika kutangaza Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania ulitumia fursa hiyo kutangaza fursa za Uwekezaji, kuhamasisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili na kutangaza vivutio vya Utalii kwa kuonesha Filamu ya The Royal Tour.

Mhe. Chithyola akifurahia chakula cha kitanzania alipotembelea banda la Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Afrika yaliyofanyika jijini Lilongwe hivi karibuni. Wengine katika picha ni Mhe. Balozi Kayola na wageni wengine waliotembelea Banda la Tanzania.

Kadhalika Ubalozi ulishirikiana na Watanzania Diaspora wanaoishi Malawi kuonesha Utamaduni wa Tanzania ikiwemo vyakula vya asili.

Banda la Ubalozi wa Tanzania lilitembelewa na wageni wengi ambao walipendezwa na vyakula vya asili kutoka Tanzania.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Simplex Chithyola.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news