ARUSHA-Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu amekamatwa na polisi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ambapo Kamanda Justine Masejo amethibitisha kumshikilia makamu mwenyekiti huyo.
Inadaiiwa kuwa, Lissu amekamatwa leo asubuhi akiwa hotelini alipofikia eneo la Karatu Mkoa wa Arusha.
Jana mwanasiasa huyo aliingia kwenye purukushani na Jeshi la Polisi baada ya kuzuiwa alipokuwa njiani kuelekea Ngorongoro alipopanga kufanya mikutano ya hadhara.
Baada ya Polisi kuzuia msafara wake, Lissu na pamoja na watu walioambatana nao waliamua kukaa barabarani wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na safari ya kuelekea Ngorongoro.Aidha, Kamanda Masejo amesema, Jeshi la Polisi linamshikilia Lissu na wenzake kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuwazuia polisi kutekeleza majukumu yao;