Tutafanyia kazi mapendekezo ya tume-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Maboresho ya mifumo ya taasisi za Haki Jinai nchini.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Septemba 9, 2023 Ikulu jijini Zanzibar alipokutana na tume hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Balozi Ombeni Sefue walipomkabidhi ripoti ya tume hiyo.

Alieleza kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeyapokea mapendekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuleta mabadiliko na mageuzi makubwa kwa nia ya kupatikana kwa haki ufanisi.

Pia amesema,utekelezaji wa mapendekezo hayo unaendana na kutegemeana na taasisi zote za haki jinai za Tanzania Bara na Zanzibar.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Mwinyi alizungumzia kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa ya Zanzibar (ZAECA) na ya kupambana na dawa za kulevya, ambapo amrsema, taasisi hizo zimepata msaada wa kujengewa uwezo na wenzao kutoka Bara kwa kupewa mafunzo.

“Bila shaka ni sahihi kabisa lazima kuwe na kubadilishana ujuzi na uzoefu, na ushirikiano wa karibu,”alisisitiza Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi.

Kuhusu Mahakama ya Rufani Bara kufanya kazi zake Zanzibar alisema, tayari suala hilo lipo mezani na linashughulikiwa.

Naye Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Mohamed Othman Chande, alimueleza Dkt.Mwinyi kwamba tume ilifanikiwa kuzifanyia kazi changamoto za taasisi 15 zilizopendekezwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwemo Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashitaka na Jeshi la Magereza.

Taasisi nyengine ni mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa, Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, Mahakama ya Tanzania, kitengo cha kudhibiti fedha haramu, uhamiaji, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Sambamba na taasisi nyingine zinazohusu masuala ya jinai kwa kutathmni ushirikiano wa taasisi hizo na kuangalia nidhamu, mifumo ya ajira, viwango vya weledi, tume ya upandishaji vyeo, ufanisi mahusiano, nidhamu, ufanisi matumizi ya teknolojia na motisha.

Tume ya Maboresho ya Mifumo ya Taasisi za Haki Jinai imeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, Januari 31, 2023 na ilianza kazi zake mapema mwezi Februari,mwaka huu kwa lengo la kutathmni mifumo ya haki jinai na kutathmini taasisi za haki jinai.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news