Ufuatiliaji na Tathmini haviepukiki-Cosmas Ngangaji

ARUSHA-Imeelezwa kuwa,suala la Ufuatiliaji na Tathmini lina umuhimu mkubwa katika kuangalia utekelezaji wa mipango kuanzia ngazi ya mamlaka za chini hadi ngazi ya taifa katika utendaji hususani kwenye miradi ikilinganishwa na namna gani inakwenda sawasawa au inatekelezwa kama ilivyopangwa.
Bw. Cosmas Ngangaji, Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akizungumza katika siku ya pili ya Kongamano la Pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini linaloendelea jijini Arusha.

Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji katika siku ya pili ya Kongamano la Pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini linaloendelea jijini humo.

Amesema kuwa, suala la Ufuatiliaji na Tathmini linajikita zaidi katika vitendea kazi vinavyotakiwa kutumika pamoja na michakato inayotumika kama inafanya kazi na kuleta matokeo chanya hususani katika sekta ya umma.

Washiriki wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali wakati wa siku ya pili ya Kongamano la Pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini linaloendelea jijini Arusha.

Akitolea mfano wa dhana ya tathmini ya utoaji wa huduma za kijamii, Bw.Ngangaji alisema kuwa, miradi mingi ya Serikali inatakiwa kuwekewa misingi endelevu ili wananchi waweze kupata huduma sahihi na kwa wakati.

Akiongea katika kongamano hilo, Bw.Mussa Mshirazi Mbarouk kutoka Tume ya Mipango ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alisema, suala la Ufuatilijai na Tathmini ni suala linalohitaji kujifunza mara kwa mara ili kusaidia kujenga uwezo katika utendaji wa shughuli za kila siku.
Bw.Gideon Michael kutoka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma akitoa wasilisho wakati wa siku ya pili ya Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini linaloendelea jijini Arusha.

Kongamano la Pili la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini linaloendelea jijini Arusha limeingia katika siku ya pili ambapo mada mbalimbali zimeendelea kuwasilishwa.

Miongoni mwa mada hizo ni pamoja na kuimarisha uelewa wa tathmini, majadiliano bayana juu ya matokeo halisi na mbinu muhimu za kuleta mbadiliko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news