ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema mambo muhimu katika nchi yoyote la kwanza kuwa na amani pia kuendeleza utamaduni wa kuiombea na kuitunza amani, kudumisha umoja na mshikamano kwa wananchi.


Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewashukuru waumini waliojitokeza katika dua hiyo na kufarajika kuendelea kuwaombea viongozi dua ili watimize ahadi zao kwa wananchi na kusaidia nchi ipate maendeleo yanayotarajiwa.
Vilevile, amewahimiza waumini hao kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kuhusu suala la mmong'onyoko wa maadili katika jamii hivyo amewataka wazazi na walezi kuwafundisha elimu ya dini watoto na vijana wawe na hofu ya Mungu kwa ngazi ya familia katika malezi ili waweze kuwa na maadili mema.