Watunishiana misuli, DC Malenya aingilia kati

RUVUMA-Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Ngollo Malenya anatarajia kuunda tume itakayoshughulikia kuchunguza malalamiko ya wananchi kuhusu uuzaji wa maeneo ya vijiji.
Malenya amefika uamuzi huo kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Songambele.

Ni baada ya wananchi wa kijiji hicho kuutuhumu uongozi wa kijiji hicho kuhusika na uuzaji wa maeneo ya kijiji hicho huku uongozi wa kijiji hicho kukana kuhusika na uuzaji huo.

Mustafa Maleka mkazi wa Kijiji cha Songambele alimwambia mkuu wa wilaya ya Namtumbo kuwa uongozi wa kijiji hicho umehusika kuuza maeneo ya kijiji bila kufuata utaratibu.

Naye Maleka Adam Maleka mkazi wa Kijiji cha Songambele alimwambia mkuu wa wilaya kuwa, mwenyekiti wa kijiji hatoi majibu sahihi kuhusu msitu uliouzwa na kuharibiwa wa kijiji hicho.

Aidha, mzabuni Maleka mkazi wa Kijiji cha Songambele alidai, mwenyekiti huyo alisimamishwa katika nafasi yake kutokana na tuhuma za kushindwa Kutoa majibu ya uuzaji wa maeneo ya kijiji hicho, "hivyo tunashangaa kumuona akiwa anaongoza mkutano tena,"alisema Maleka.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Songambele, Omari Magazini alimwambia mkuu wa wilaya kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake na uongozi wake hazina ukweli wowote bali familia ya Maleka ni familia iliyokuwa inajihusisha na tabia ya ki- Al- Shabab katika kijiji hicho.

Magazini alisema, wakati wa operesheni uliofanywa na Serikali kuhusu watu wanaojihusisha na tabia ya ki-Al-Shabab kijiji hicho cha Songambele kilitaja familia hiyo kujihusisha na Al Shabab hali iliyoibua chuki kwake.

Pamoja na hayo Mkuu wa wilaya alitoa nafasi kwa viongozi na wananchi kuzungumzia tuhuma zinazomkabili mwenyekiti huyo ikaonesha baadhi ya wananchi kuunga mkono kuuzwa kwa maeneo ya kijiji hicho.

Aidha,baadhi ya wananchi walionekana kupinga kuuzwa Kwa maeneo hayo kwa madai kuwa maeneo hayo yamevamiwa na wafugaji ambao hawana vibali ya kukaa katika maeneo hayo huku wengine wakidai viongozi wamewauzia.

Kufuatia sintofahamu hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo aliwaambia wananchi hao kuwa ataunda tume ya kuchunguza malalamiko hayo ili viongozi wanaokumbatia wafugaji wakibainika kufanya hivyo kutoka kwenye taarifa ya tume watashughulikiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya anafanya ziara ya kuzungumza na wananchi katika vijiji vya wilaya hiyo kwa kusikiliza kero za wananchi na kisha kuzipatia majawabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news