Zanzibar kutoa vitambulisho 25,000 vya wazee wote wanaopokea pensheni jamii

NA SALMA LUSANGI
WMJJWW Zanzibar

WAZIRI wa Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Zanzibar, Mhe. Riziki Pemba Juma amesema wizara hiyo inatarajia kutoa vitambulisho 25,000 vya wazee wote wanaopokea pensheni jamii ili viweze kutumika katika huduma mbalimbali ikiwemo wakati wa kupokea pensheni jamii.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Riziki Pembe Juma akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maoni, ushauri na mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi, katika kikao cha 8, mkutano wa 12 wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani Mjini Unguja, siku ya Septemba 22, 2023.

Kauli hiyo ameitoa Septemba 22, 2023 wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maoni, ushauri/ mapendekezo ya kamati ya kudumu ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar mwaka wa fedha 2022/2023, huko Chukwani, Unguja.

Amesema, jumla ya vitambulishoa 25,000 vinatarajia kupatikana katika mwaka wa fedha 2023/2024 ambavyo watapewa wazee wote wanaopokea pensheni jamii.

Amesema, Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumza za SMZ wanaendelea na utaratibu wa kuwatengenezea vitambulisho hivyo.

Hata hivyo, Waziri huyo amesema jumla ya vitambulisho 3,668 tayari vimeshatolewa kati ya walengwa 28,776 hadi kufikia mwezi Juni, mwaka huu.

Aidha, amesema wizara yake imetoa mafunzo ya utoaji wa huduma za mpango wa pensheni jamii kwa masheha wapya 31 wa Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja na masheha 30 wa wilaya Wete na Micheweni, Pemba ikiwa ni juhudi za kuwajengea uwezo katika utowaji wa huduma za pencheni jamii.

Amesema, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatumia njia mbali mbali kuelimisha jamii elimu inayohusiana na pensheni jamii kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo, Facebook, Twitter, Instagram na Youtube pamoja na kushiriki katika matamasha ya maonesho mbalimbali.

Wakati huo huo amesema wizara yake imekamilisha uhakiki wenye lengo la kujiridhisha uwepo wa wazee hivyo, jumla ya wazee 11,850 kwa upande wa Unguja, na wazee 4,388 ni wanufaika wa Mpango wa pencheni jamii.

"Uhakiki huo ulifanyika nyumba kwa nyumba kwa upande wa Unguja katika wilaya zote na Pemba kwa wilaya ya Mkoani, Wete na Micheweni,, hivyo tumejiridhisha uwepo wa wazee wanaonufaika na mpango wa pensheni jamii,"amesema Waziri Pembe.

Sambamba na hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar mwaka wa fedha 2022/2023, Mhe. Sabiha Filfil Thani amesema, kamati hiyo inaipongeza Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuweza kukamilisha zoezi la uhakiki wa wazee wanaonufaika na pencheni jamii , pamoja utengenezaji wa vitambulisho.

“Mheshimiwa Spika katika kukuza hadhi na majukumu ya Idara ya Ustawi wa Jamii na Jinsia kamati ilishauri wizara kuharakisha upatikanaji wa vitambulisho vya wazee waliyofikia umri.

"Kamati inaishukuru wizara kwa kupokea ushauri huo na kuufanyika kazi kuanza kuwapatia wazee vitambulisho hivyo,”alisema Thani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news