DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameilekeza Bodi ya Filamu nchini ishirikiane na sekta binafsi katika kuhakikisha filamu za Tanzania zinakua bora zaidi na zinapata soko la uhakika.

Ameitaka bodi hiyo ibadilike na kwenda na wakati ili kupanua wigo wa kuwahudumia wadau wake kibiashara na kuongeza mapato.