DAR ES SALAAM-Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imetoa taarifa ya ufafanuzi na tamko juu ya taarifa inayohusu ndugu Mwemba Mwemba Burtony (Mwijaku) kuhusu kutumiwa na TTB nchini Ufaransa kutangaza utalii nchini.
"Bodi ya Utalii Tanzania inakanusha kuwa, haijamtumia wala kumtuma mtajwa hapo juu (ndugu Mwijaku) kutangaza utalii huko nchini Ufaransa akiwa balozi wa utalii kwa niaba au kwa gharama za Serikali (TTB);