Bunge la Tanzania, UNDP wasaini andiko la Mradi wa LSP III

DAR ES SALAM-Bunge la Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wamesaini Andiko la Mradi wa Awamu ya Tatu wa Kuwajengea uwezo Waheshimwa Wabunge na Watumishi wa Bunge (LSP III) wenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00. Aidha, Mradi huo utahudumia pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Ndg. Sergio Valdini wakisaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi akishuhudia tukio hilo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndg. Sergio Valdini katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Oktoba, 2023.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Ndg. Sergio Valdini wakisaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi akishuhudia tukio hilo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akibadilishana hati na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Ndg. Sergio Valdini mara baaada ya kusaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Andiko hilo limesainiwa leo tarehe 11 Oktoba, 2023 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam ambapo Utekelezaji wa Mradi huo utaanza Mwezi Oktoba 2023 hadi Novemba 2027.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news