Bunge lakaribisha maoni Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika wa 2019

DODOMA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imepanga kufanya Mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu Azimio la Bunge la Mapendekezo ya Kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika wa Mwaka 2019 (Treaty for the Establishment of the African Medicines Agency – AMA).
 Hayo ni kwa mujibu wa taraifa iliyotolewa kwa umma na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

Kamati inatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa Kanuni ya 108 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023.

Kamati itasikiliza na kupokea maoni ya wadau (Public Hearing) siku ya Alhamisi tarehe 26 Oktoba, 2023 saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi Namba 9, Jengo la Utawala, Bungeni jijini Dodoma.

Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Azimio hilo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla kupelekwa katika hatua nyingine.

Vilevile Kamati itapokea maoni kwa njia ya Posta au Barua Pepe kwa anuani ifuatayo:- Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge, 10 Barabara ya Morogoro, S.L.P. 941, 41105 Tambukareli, DODOMA. Baruapepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz

"Mkataba huo unaweza kupakuliwa katika tovuti ya Bunge, www.bunge.go.tz. Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili ya hatua za kiutawala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news