CHAUMATA waandaa maonesho makubwa ya ufugaji na mazingira

DAR ES SALAAM-Chama cha Watunzaji wa Mazingira na Ufugaji wa tija Tanzania (CHAMAUTA) kimeandaa maonesho makubwa ya ufugaji na mazingira ambayo yatafanyika kwa siku sita katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma. Maonesho hayo yanatarajia kuanza Oktoba 29, mwaka huu na kuhitishwa Novemba 3,2023 jijini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHAMAUTA, Jeremiah Wambura amesema, lengo ni kuhamasisha kuwa na vyakula bora vikiwemo maziwa.

Amesema kuwa, wafugaji 60 wamepimiwa maeneo yao na wanatarajiwa kupewa hati Novemba 3,2023 ili kuzuia mifugo yao kuzurura.

"Tunashukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule kwa kutoa sapoti,kwani amekuwa msaada mkubwa kwetu,"amesema Wambura.

Ametoa wito kwa serikali na wadau nchini kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kuwaunga mkono waandishi ambao wanafanya kazi kubwa ya kuhabarisha umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news