David Massamba Memorial Secondary School yaanza kujengwa rasmi

NA FRESHA KINASA

HATIMAYE ujezi wa David Massamba Memorial Secondary School umeanza rasmi katika Kijiji cha Kurwaki kilichopo Kata ya Mugango katika Jimbo la Musoma Vijijni mkoani Mara.

Ujenzi huo umeanza Oktoba 23, 2023 ukiwa ni uamuzi wa kuenzi kazi na mafanikio makubwa ya mbobezi wa lugha ya Kiswahili marehemu Prof.David Massamba, baada ya Agosti 30, mwaka huu waombolezaji akiwemo Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof.Muhongo kuridhia uamuzi huo.

Siku hiyo ndio ambayo nguli huyo wa Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi alipumzishwa nyumbani kwake penye utulivu na amani ya milele.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Oktoba,23 mwaka huu. Huku ikisema kuwa,

"Matayarisho ya kuanza ujenzi yamekamilika na kiwanja cha uhakika na kikubwa kimepatikana kwenye Kitongoji cha Kati kijijini Kurwaki.

"Michoro ya majengo imetolewa na halmashauri yetu (Musoma DC). Eneo la ujenzi (kiwanja) limekidhi vigezo vyote hitajika."

MATUNDA YA HARAMBEE ILIYOFANYIKA OKTOBA 2,2023

"Harambee ya kwanza ya Oktoba 2, 2023 iliyofanyika kijijini Kurwaki imefanikisha upatikanaji wa saruji mifuko 481 (ikiwemo Mifuko 250 ya Mbunge wa Jimbo, na Mifuko 50 kutoka kwa Wajukuu wa Hayati Mzee Korogo wa kijijini Kurwaki, mchanga lori 45 na mawe lori 31 na Fedha taslimu ni sh ilingi 615,000 (zikiwemo sh.500,000 kutoka kwa Familia ya Hayati Prof.David Massamba," imeeleza taarifa hiyo.

"Akaunti ya Benki ya kuweka mchango wako ni hii hapa: Serikali ya Kijiji cha Kurwaki Benki: NMB namba: 30302301539. Tunakukaribisha sana uungane nasi kumuenzi aliyekuwa bingwa Mkuu wa Lugha ya Kiswahili Hayati Prof. David Massamba,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, wananchi wamepokea kwa furaha na shauku kubwa ujenzi wa shule hiyo huku wakimpongeza Prof. Muhongo kwa maono mazuri ambayo aliwashirikisha na wao kuyapokea kwa mikono miwili na kuyafanyika kazi kwa kuchangia ujenzi huo kwani utasaidia kuwaondolea changamoto wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda masomoni.

Mbunge Prof. Muhongo amesema kuwa, Desemba, mwaka huu itafanyika harambee kubwa ya kufa na kupona ya uchangiaji wa shule hiyo ambapo matarajio ifikapo Januari 25, mwaka ujazo shule hiyo ianze.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news