DCEA,TAKUKURU wabisha hodi shuleni na vyuoni nchini

DODOMA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) wamezindua Mwongozo wa Utoaji Elimu na Kampeni ya Kutokomeza Rushwa na Dawa za Kulevya shuleni na vyuoni.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma na ulikwenda sambamba na mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo maafisa TAKUKURU kutoka mikoa mbalimbali nchini.

"Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwa na uelewa wa pamoja kati ya maafisa wa TAKUKURU na maafisa wa DCEA na kupata namna bora na mbinu sahihi ya kufikisha elimu katika klabu zinazopatikana shuleni na vyuoni juu ya tatizo la dawa za kulevya na rushwa kwa ujumla.

"Tatizo la dawa za kulevya lina mahusiano ya karibu na tatizo la rushwa, kwa kuwa yote ni makosa ya kupangwa, yote yanahitaji suluhu zinazofanana ambazo ni elimu sahihi kwa umma, juu ya madhara ya dawa za kulevya na madhara ya rushwa katika Taifa na katika jamii kwa ujumla.

"Nipende kutoa wito kwa wadau wote,maafisa wa mamlaka ya dawa za kulevya, maafisa wa TAKUKURU,walimu wa shule na vyuo, klabu, wanachama, waandishi wa habari, wasanii, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi wote kwa ujumla kushiriki nasi katika kukamilisha malengo yetu ya kampeni hii,"amefafanua kwa kina Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo. Endelea kusikiliza zaidi video hapa chini;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news