Dkt.Mpango asisitiza kujenga uchumi shindani wa viwanda

NJOMBE-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango tarehe 28 Oktoba, 2023 amehitimisha rasmi Maonesho ya Shirika la Viwanda vidogo vidogo (SIDO) yaliyofanyika katika Viwanja vya Sabasaba katika Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga wakitembelea Mabanda ya Maonesho ya Wajasiliamali katika Viwanja vya Sababa Mkoani Njombe tarehe 28 Oktoba, 2023.

Dkt. Philip Mpango aliwasili viwanjani hapo na kuanza kutembelea mabanda mbali
mbali ya maonesho ya bidhaa za Wajasiliamali hao na kujionea ubunifu tofauti katika
Sekta ya Viwanda hapa nchini.

"Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano tunaoutekeleza hivi sasa unatutaka tukuze mchango wa Uchumi pamoja na Ajira zinazotokana na Viwanda katika pato la Taifa. "Hivi sasa mchango wa Sekta ya Viwanda ni asilimia 7.1 tunatamani tufikie asilimia 9 ifikapo mwaka 2025 hadi 2026,"amesema Dkt.Mpango.

Dkt.Mpango amesisitiza kuwa, tafiti zina umuhimu mkubwa sana katika kukuza
matumizi ya teknolojia mbali mbali kwenye Uzalishaji na uongezaji thamani wa bidhaa na mazao.
Katika Maonesho hayo ambayo Tume ya Madini ilishiriki, akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Tume ya Madini. Dkt. Mpango amewataka Watendaji wa Tume ya Madini kufanya utafiti ili kujua madini yapi yanapatikana eneo gani? na kuhakikisha takwimu mbalimbali zinapatikana hapa nchini ili kuongeza Pato la Taifa.

Dkt.Mpango amesema kuwa, maonesho ya SIDO yameshirikisha Wajasiliamali 628 na
teknolojia 95 ambazo zinatumika kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao mbali
mbali ikiwemo Parachichi linalozalishwa kwa wingi Mkoani Njombe.

Aidha, Dkt Mpango ameelezea kufurahishwa kwake na kauli mbiu ya Maonesho hayo
ambayo inasema;"Kwa Pamoja tujenge Viwanda kwa Uchumi na Ajira endelevu" na kusema, Kauli hii iwahamasishe watu wote hasa vijana kuingia kwenye Sekta ya Kilimo,Viwanda na Biashara.
Akizungumza katika Maonesho hayo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema, Maonesho ya nne ya Wajasiliamali yamekuwa na ongezeko
kubwa la washiriki ambapo mwaka 2018 walihudhuria Wajasiliamali 582 yalipofanyika kwa mara ya kwanza Mkoani Simiyu na mwaka 2023 idadi ya washiriki imeongezeka kufikia Washiriki 628.

Hafla ya kilele cha Maonesho hayo ambayo yamefikia tamati tarehe 28 Oktoba, 2023,
yamehudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Sekta Binafsi, Viongozi wa dini,
Wajasiliamali pamoja na Wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news