Dkt.Possi ahimiza kasi Meli ya MV Mwanza na MT Sangara

MWANZA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya UChukuzi, Dkt.Ally Possi ameutaka uongozi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuongeza kasi zaidi ya kuwasimamia wakandarasi wa Gas Entec anayejenga Meli ya MV MWANZA iliyopo Bandari ya Mwanza Kusini na KTMI CO- LTD anayekarabati Meli ya MT SANGARA iliyopo Bandari ya Kigoma
Dkt.Possi amezungumza hayo jijini Mwanza, katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea chini ya Usimamizi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).

Dkt Possi amesema Bado hajaridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi meli mpya ya MV. MWANZA inayotekelezwa katika Bandari ya Mwanza Kusini ambapo hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 88.

"Bado sijaridhishwa na Kasi ya ujenzi wa Meli hii mpya ya MV MWANZA hivyo nawataka wasimamizi wa mradi huu kuusimamia Kwa Kasi zaidi ili uende kukamilika Sasa na kwa thamani halisi ya fedha" amesisitiza Dkt Possi

Kwa upande wa ukarabati wa Meli ya Mafuta ya MT SANGARA unaendeleaje kwenye Bandari ya Kigoma iliyopo Ziwa Tanganyika Dkt Possi amesema amepokea taarifa kutoka Kwa Uongozi kuwa ukarabati wake umefikia asilimia 92 na kusisitiza uongezwe Usimamizi ili ukarabati huo ukamilike kabla ya mwisho wa mwaka huu

"Nimepokea taarifa ya ukarabati wa Meli yetu ya kubeba mafuta ya Mt SANGARA ambao umefikia asilimia 92, Sasa natoa rai twende tukamilishe Sasa kwani Meli hii ni muhimu sana Kwa Usafirishaji wa mafuta hata Kwa Nchi jirani za Burundi na Drc Congo" amesema Dkt possi.

Akitoa taarifa ya miradi inayoendelea kutekelezwa chini ya Usimamizi wa Kampuni, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Eric Hamissi, amesema kuwa Kampuni hiyo Kwa Sasa inatekeleza Miradi miwili ambao ni ujenzi wa Meli mpya ya Mv Mwanza inayoendelea kwenye Bandari ya Mwanza Kusini ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 88 na utatumia shilingi Bil 109 mpaka kukamilika mwanzoni mwa mwaka ujao na Ukarabati wa Meli ya Mafuta ya Mt SANGARA unaendelea kwenye Bandari ya Kigoma iliyopo Ziwa Tanganyika ambayo imefikia asilimia 92 na utatumia shilingi Bil 8.3 mpaka kukamilika

Bw. Eric amesema ujenzi wa meli ya Mv Mwanza itakayokuwa na madaraja matatu, maeneo ya watu mashughuli (VIP), vyumba vya mikutano, uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 na magari madogo 20 unaotekelezwa na Mkandarasi Gas Entec wa Korea Kusini unaendelea sambamba na ule ukarabati Meli ya Mt SANGARA yenye uwezo wa kubeba Lita 410,000 sawa na Tani 350 za mafuta utasaidia sana Kampuni kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi Kwa ukubwa zaidi

Aidha, ameeleza changamoto iliyokabili mradi huo kuchelewa ni kutokana na kuanza ujenzi wa meli bila ya kuwa na chelezo Kwa miezi sita ambapo sasa ujenzi wa chelezo umekamilika na kazi zinaendelea.

Naye, Meneja wa Mradi Luteni Kanali Mhandisi Vitus Mapunda, amemuhakikishia Naibu Katibu Mkuu kuwa ujenzi wa meli hiyo unasimamiwa kwa karibu na kwa viwango vinavyohitajika katika meli za aina hiyo.

Ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza unatekelezwa na Kampuni ya Gas Entec Company Limited ikishirikiana na kampuni ya Kangnam Corporation zote kutoka Korea Kusini zikishirikiana na SUMA JKT ya Tanzania ambapo mradi unatarajiwa kukamilia mwanzoni mwa mwaka ujao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news