Hali ya lishe imeimarika nchini-Dkt.Yonazi

ARUSHA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Masuala ya Lishe wa mwaka 2021-22-2025/26 umekuwa na mafanikio makubwa kutokana na juhudi za pamoja za wadau wa lishe nchini na kupelekea kuimarika kwa kiasi kikubwa kwa hali ya lishe na kupungua kwa viwango vya utapiamlo kwa baadhi ya viashiria.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kushoto),Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe wakiwasili kushiriki mkutano wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha tarehe 25 Oktoba, 2023.Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni: “Kuimarisha Mifumo ya Chakula kwa Matokeo Bora ya Hali ya Lishe na Maendeleo ya Rasilimali Watu na Ukuaji wa Uchumi,"

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Lishe nchini unaofanyika Jijini Arusha katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Mount Meru tarehe 25 Oktoba, 2023, Dkt. Yonazi amesema kupitia mkutano huo utaweza kujadili mafanikio hayo na kuona uwezekano wa mikoa mingine kutumia mbinu zilizotumika katika mikoa iliyopata mafanikio na dhairi kuwa kasi ya kupungua viwango vya udumavu kwa watoto nchini itaongezeka

Dkt. Yonazi amesema kiwango cha Udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambacho ndiyo kiashiria kikuu cha Utapiamlo kimepungua kutoka asilimia 34 mwaka 2016 hadi asilimia 30 mwaka 2022 na tathmini imeonesha kuwa mikoa saba imefanikiwa kupunguza vinwango hivyo kwa watoto zaidi ya asilimia 10 katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2022.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu kushoto (kwake) pamoja na wajumbe wa meza kuu wakifuatilia Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe akizungumza wakati wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe uliofanyika Jijini Arusha.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu wakati wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe uliofanyika Jijini Arusha.

“Mafanikio mengine yanajumuisha kupungua kwa kiwango cha ukondefu kutoka asilimia 3.8 mwaka 2016 hadi asilimia 3.5 mwaka 2022 pamoja na kupungua kwa tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa wanawake walio katika umri wa uzazi (miaka 15 hadi 49) kutoka asilimia 44.8 mwaka 2015 hadi asilimia 28.8 mwaka 2018,” alisema Dkt. Yonazi.

Aidha, Dkt. Yonazi amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana kupitia Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Masuala ya Lishe wa mwaka 2021-22-2025/26, amesema bado kuna changamoto ambazo zimeendelea kuongezeka ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya watoto wenye udumavu ambapo takwimu zinaonesha kuongezeka kutoka 2,700,000 mwaka 2016 hadi kufikia 3,400,000 mwaka 2022.

“Ni wajibu wetu sote katika mkutano huu kuhakikisha mikakati na maazimio tutakayoyafikia yanalenga kupunguza changamoto zinazotukabili katika utekelezaji wa Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe, ikiwemo changamoto ya kuongezeka kwa idadi ya watoto wenye udumavu,"alisema Dkt. Yonazi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula an Lishe Nchini (TFNC) Dkt. Ray Masumo (kushoto)pamoja na Mkurugenzi Idara ya Lishe, Sera na Mipango TFNC Dkt. Japhet Mtaturu wakifuatilia hoja wakati wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia mimea ya protini alipotembeela banda la ECHO wakati wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe uliofanyika Jijini Arusha.Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe wakifuatili mawasilisho wakati wa mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe wakifuatili mawasilisho wakati wa mkutano huo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa sektarienti ya maandalizi ya Mkutano Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Wadau wa Lishe.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Akitoa salamu za kwa niaba ya Wadau wa Lishe nchini, Mkuu wa Shughuli za Lishe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Patric Codjia, amesema wataendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha masuala ya lishe yanaendelea kuimarika na kuyafikia malengo yaliyopo.

“Tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu wa Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwa matokeo Chanya katika kuhakikisha masuala ya lishe yanapewa kipaumbele na kuwa na matokeo tayarijiwa na tumefarijika kuwa sehemu ya kongamano hili la wadau wa masuala ya Lishe,” alisema Patric

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news