DAR ES SALAAM-Baada ya kuimarisha huduma mbalimbali ikiwemo kuweka puto Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa watu wanaopenda kupungua uzito sasa huduma hii pia imeanza kutolewa MNH-Upanga.

Dkt. Kitembo amesema kuwa mwishoni mwa wiki hii tayari mtu mmoja amepata huduma hiyo MNH-Upanga ambapo MNH-Mloganzila watu 150 wameishahudumiwa tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mwishoni mwa mwaka jana 2022.