Israel yatuhumiwa kuua Wapalestina 400 ndani ya saa 24

GAZA-Raia 400 wa Palestina wanadaiwa wameuawa kikatili na karibu wengine 1500 wamejeruhiwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Mauaji hayo ambayo yanatajwa kutokea Oktoba 14, 2023 inadaiwa ni wakati mauaji ya halaiki yanayotekelezwa na jeshi la Israel yalipopamba moto katika Ukanda wa Gaza ambao wanauzingira.

Mwandishi wa WAFA aliripoti kuwa, jeshi la Israel lilifanya mfululizo wa mashambulizi ya anga yaliyolenga nyumba 10 zinazokaliwa na watu huko Deir al-Balah katikati mwa Gaza. Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 80 na wengine 250 kujeruhiwa.

Katika mji wa Gaza, takribani raia 260 waliuawa chini ya mashambulizi makali ya Israel dhidi ya vitongoji vya Tal al-Hawa, Al-Rimal, na kambi ya wakimbizi ya Shati', pamoja na kitongoji cha Shejaiya na Al-Zaytoun katika sehemu ya Mashariki ya mji huo. .

Aidha, katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, wakaazi wapatao 40 walipoteza maisha huku mashambulizi ya anga ya Israel yakiangusha nyumba zilizokuwa na wakaazi ndani.

Zaidi ya hayo, takribani raia 10 waliuawa kikatili katika mji wa Beit Lahiya uliopo Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi makubwa ya Israel yaliyolenga nyumba kadhaa.

Huko Khan Yunis, Kusini mwa Ukanda wa Gaza, takribani raia 20 waliuawa huku ndege za kivita za Israel zikilenga majengo ya makazi na raia ndani.

Kwa mujibu wa WAFA, mashambulizi hayo ya anga sio tu yalisababisha hasara kubwa ya maisha, lakini pia yalisababisha uharibifu mkubwa kwa miundombinu ya maeneo yaliyolengwa, huku makumi ya nyumba na majengo ya makazi yakiharibiwa. Aidha, hali bado ni mbaya huku juhudi za uokoaji zikiendelea katikati ya uvamizi huo unaoendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news