Jawaharlal Nehru University kumtunuku Rais Dkt.Samia udaktari wa heshima

NEW DELHI-Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mheshimiwa January Makamba amesema, Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kilichopo New Delhi nchini India kitamtunuku shahada ya heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Ni kwa kutambua mchango wake katika diplomasia ya uchumi, mafanikio katika kusukuma maendeleo yanayogusa watu moja kwa moja na mafanikio katika kuimarisha mahusiano ya Kimataifa kwa ujumla kwenye Umoja wa Mataifa (UN).

Waziri Makamba ambaye yupo nchini India katika ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia amesema,chuo kikuu hicho kimefikia uamuzi huo baada ya kutambua mchango wa Rais Dkt.Samia kwenye kuunganisha India na Tanzania.

“Tumepata taarifa rasmi kuwa Chuo Kikuu kinachoheshimika hapa India cha Jawaharlal Nehru kimeamua kumtunuku Rais wetu Degree ya Heshima ya Udaktari.

"Shughuli hii itafanyika Oktoba 10,2023,chuo hiki ni namba moja wamesoma watu muhimu hapa akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje sasa hivi, Waziri wa Fedha na wengine wengi.

"Sisi tunashukuru Mheshimiwa Rais anatambuliwa, anatambulika na anaheshimika hata kwenye mataifa mengine kwa kazi kubwa anayofanya katika mataifa mengine,”amesema Waziri Makamba. 
 
Jawaharlal Nehru ni chuo kikuu cha utafiti wa umma kilichopo Kusini Magharibi mwa New Delhi, India. Kilianzishwa mwaka 1969 na kikapewa jina la Jawaharlal Nehru, Waziri Mkuu wa kwanza wa India.

Chuo kikuu hicho kinajulikana kwa vitivo vinavyoongoza na msisitizo wa utafiti juu ya sayansi ya kijamii na sayansi shirikishi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news