DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida Rashid Abdallah amewataka watoto wa kike wenye ulemavu kutoona hali hiyo kwamba ni kikwazo cha kutosoma na kukatisha ndoto zao za maisha.
Hafla hiyo iliandaliwa na Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu,Naibu Katibu Mkuu amesema, anaelewa changamoto zinazowakabili wasichana hao, lakini hawatakiwi kukataa tamaa katika kutafuta elimu ili wawe viongozi wa baadae.

Amesema, nchi ya Tanzania ina miongozo mbalimbali ambayo inasimamia masuala ya watu wenye ulemavu ikiwemo UN Convection on the Right of People with Disability.
Pia amesema, kuna sheria ya Tanzania Bara ya 2010 kwa upande wa Zanzibar kuna sheria namba 9 ya mwaka 2006 ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka jana, sheria zote hizo zinazungumzia wajibu wa utambuzi wa haki kwa watu wenye ulemavu, usawa na kutokubaguliwa, kukuza uelewa, n.k.

Aidha, Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa walimu wote katika skuli mbali mbali kuweka vyoo rafiki kwa Watoto wenye ulemavu, na sio vyoo tuu hata njia ili mazingira nayo yawe rafiki ili wajihisi wako na amani.
Naye Mkurugezi wa Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu, Sofia Mbeyela amesema, mradi huyo wa ujenzi wa vyoo rafiki kwa Watoto wa kike wenye ulemavu umeanza Julai mwaka jana na umegharibu milioni 20,000 kwa kujenga vyoo vine na chumba kimoja kwaajili ya wasichana hao kubadili nguo wakati wakiwa katika siku zao za hedhi.

Amesema, mradi huo utaendelea kwa skuli zote hivyo amewaomba wananchi, viongozi, mashirika/taasisi za umma na Serikali kuendelea kuchangia mradi huo ili kuwaondolea Watoto wenye ulemavu changamoto hiyo.

Mkurugezi wa Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu, Sofia Mbeyela na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Abeida Rashid Abdallah ni watu weneye ulemavu, hivyo wanaelewa changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu na wataendelea kupambana ili kuhakikisha watu wenye ulemavu hawajaachwa nyuma.