Kila Mtanzania ana fursa ya kujiunga na huduma zetu-NHIF

DODOMA-Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema kila Mtanzania anayo fursa ya kujiunga na huduma zake na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote bila kikwazo cha fedha.

Ili kuwezesha hilo, Mfuko umehakikisha kila kundi au mwananchi mmoja mmoja amewekewa utaratibu unaomuwezesha kujiunga.

Makundi hayo ni pamoja na kundi la Watumishi wa Umma ambao wanajiunga kwa mujibu wa Sheria ambapo Mtumishi anajiunga na mwenza wake pamoja na wategemezi wake wanne ambao ni watoto wake ambao watahudumiwa mpaka umri wa miaka 21, wazazi wake na wakwe.

Mfuko pia umeweka utaratibu wa kundi la wanafunzi kuanzia elimu ya Msingi hadi elimu ya Vyuo vya Juu na Kati ambao wanajiunga kupitia shule ama vyuo wanavyosoma kwa mchango wa Shilingi 50,400 kwa mwaka.

Kwa upande wa watoto ambao hawajaanza shule wanayo fursa ya kunufaika na huduma za Mfuko kupitia mpango wa Vifurushi ambapo wazazi wao wanaweza kujiunga nao kama wategemezi.

Kwa upande wa wananchi wanaojiunga kibinafsi, Mfuko una mpango wa Vifurushi ambao unamuwezesha mwananchi mmoja mmoja ama familia yake kujiunga na kunufaika na huduma za matibabu katika vituo vyote vilivyosajiliwa na Mfuko Tanzania Bara na Zanzibar.

Mpango wa Vifurushi unampa kila mwananchi fursa ya kujiunga na uchangiaji umezingatia mahitaji ya mhusika na hali halisi ya gharama za matibabu.

Kutokana na haya, Mfuko unawahamasisha wananchi wote kutumia fursa hii kujiunga ili kuondokana na changamoto za kukosa matibabu kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news