Kocha Mkuu wa Simba SC afichua siri kutinga hatua ya makundi Afrika

DAR ES SALAM-Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba,Roberto Oliviera (Robertinho) amesema, lengo la kwanza lilikuwa kuhakikisha timu inaingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa kuitoa Power Dynamos na hilo limefanikiwa.
Pia, Kocha Robertinho amewapongeza wachezaji kwa kutokata tamaa hadi mwisho kwa kuwa Power Dynamos ni timu bora na ilikuwa imejipanga vizuri.

Akizungumzia mchezo huo uliopigwa leo Oktoba 1, 2023 katika Dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Robertinho amesema, ilibidi kumuingiza nahodha John Bocco kipindi cha pili.

Ni baada ya kuwaona Dynamos wote wamerudi nyuma na waliziba mianya ya kupitisha pasi, hivyo alitakiwa mtu wa kusimama na walinzi wao.

“Nimefurahi kwa hatua hii, nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliofanya. Nawashukuru mashabiki,waandishi wa habari na kila mtu kwa kufika hatua hii.

“Baada ya wenzetu kupata bao walirudi nyuma wote ikawa ngumu kupitisha mipira ikabidi tumuingize Bocco kwa kuwa ni mrefu na angeweza kucheza sambamba nao na tuliongeza kasi iliyosababisha kupatikana kwa bao la kusawazisha,” amesema Robertinho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news