Kongamano la Kimataifa la magonjwa ya mishipa ya fahamu kufanyika MNH-Mlonganzila

DAR ES SALAAM-Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili na Chama cha Wanasayansi wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu Tanzania (TNA) wameandaa Kongamano la Kimataifa la 14 katika wa Ukanda Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Lengo ni kutoa mafunzo ya kukabiliana na magonjwa ya mishipa ya fahamu ikiwemo kiharusi, kifafa, maambukizi kwenye mishipa ya fahamu, magonjwa ya dharura ya mishipa hiyo na magonjwa mingine ambayo bado yana wataalamu wachache barani Afrika.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa TNA na Profesa wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu Prof. William Matuja wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa takwimu za Tanzania zinaonesha kuna wataalamu wa mishipa ya fahamu 14 tu ambapo kati yao 11 ni wa upande wa watu wazima na wa watatu ni wa upande wa watoto ikiwa ni idadi ndogo ukilinganisha na idadi ya Watanzania kwa sasa

Prof. Matuja amesema kongamano hilo litafanyika kuanzia Oktoba 28 hadi 31, 2023 MNH-Mlonganzila na kuhudhuriwa na washiriki 150 kutoka hospitali za Mikoa yote nchini ikiwemo MNH, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Hospitali ya Benjamini Mkapa, Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Hospitali ya KCMC, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya Rufaa-Mbeya, Hospitali ya Kibong’oto, Hospitali ya Mirembe na

Ameongeza kuwa washiriki wengine watatoka nchi 20 Barani Afrika ikiwemo Angola, Benin, Burkina Faso, Congo DR, Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Kenya, Madagascar, Mali, Mozambique, Niger, Nigeria, South Africa, Senegal, Togo, Uganda, Zambia na Zimbabwe

Prof. Matuja amesema magonjwa ya mishipa ya fahamu na vifo vinavyoambatana nayo yanazidi kuongezeka siku hadi siku. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa kila sekunde arobaini (40) binadamu mmoja hukumbwa na ugonjwa wa kiharusi na kila sekunde tatu 3.5 kifo hutokea kutonana na ugonjwa huo.

Prof. Matuja amesema, mojawapo ya mkakati wa kukabiliana na uhaba wa wataalamu ni pamoja na kuwapatia mafunzo madaktari na wataalamu wengine ili kuweza kutambua na kutibu magonjwa ya mishipa ya fahamu hivyo juhudi hizi zitasaidia madaktari wetu ili wakirejea kwenye maeneo yao ya kazi waweze kuwapatia huduma wagonjwa wa namna hii kwa ufanisi zaidi.

Kutakuwa na wazungumzaji kutoka vyama 9 vya magonjwa ya mishipa ya fahamu vya kimataifa kutoka Ulaya, Africa na Marekani watakaoshirikiana na wakufunzi kutoka Chama cha Wanasayansi wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu Tanzania (TNA) katika kutoa mafunzo hayo. Mashirika hayo ni Pamoja na (EAN, AFAN, AAN, IBRO, IHS, ILAE, MDS PAUNS na WFN).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news