Lengo la African Football League (AFL) ni kuzisaidia klabu za Afrika kiuchumi-CAF

DAR ES SALAAM-Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Patrick Motsepe amesema, lengo la michuano ya African Football League (AFL) ni kuzisaidia klabu za Afrika kiuchumi.

Motsepe amesema timu zinazoshiriki michuano hiyo zinapatiwa kiasi kikubwa cha fedha na zile zinazofanya vizuri zaidi kiwango iknakuwa kikubwa ambacho kinaweza kusaidia kufanya vitu vikubwa zaidi.

Motsepe ameongeza kuwa, AFL haitaiua michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kama wengi wanavyodhani badala yake imeanzisha ili kuziongezea klabu uwezo wa kiuchumi.

“Moja ya malengo ya AFL ni kuzisaidia klabu kiuchumi sababu tunalipa kiasi kikubwa, mipango yetu ni kuzifanya klabu za Afrika zijiendeshe kisasa.

“Idadi kubwa ya wachezaji kutoka Afrika wanatamani kucheza soka barani Ulaya sababu ya malipo mazuri nasi tunataka Afrika tufike kwenye hatua hiyo,”amesema Motsepe.

Motsepe amethibitisha mwakani michuano ya African Football itashirikisha timu 24 badala ya nane ambazo zitashiriki msimu huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news