Maelfu waandamana mjini Dublin kupinga uchokozi usiokoma wa Israel dhidi ya Gaza

DUBLIN-Maelfu ya waandamanaji waliingia barabarani Oktoba 14,2023 katika mji mkuu wa Ireland, Dublin, wakilaani uchokozi wa kikatili wa Israel dhidi ya Gaza na kuonesha mshikamano wao na watu wa Palestina.

Maandamano hayo yalishuhudia miungano mbalimbali ya washiriki, wakiwemo wanachama wa Jumuiya ya Palestina, jumuiya za Waarabu na Kiislamu, Kampeni ya Mshikamano wa Palestina ya Ireland, vyama vya wafanyakazi, wawakilishi wa vyama vya mrengo wa kushoto, na mamia ya watu waliosimama katika mshikamano na kadhia ya Palestina.

Waandamanaji hao wametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa ukatili wa Israel na mauaji ya kimbari yanayoendelea dhidi ya raia wasio na hatia wa Kipalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, wakisisitiza haja ya dharura ya kuweka njia za kibinadamu kwa ajili ya kusambaza chakula, maji na dawa haraka katika eneo la Gaza.

Waandamanaji hao pia wamewataka wabunge wa nchi za Magharibi kutoa mashinikizo ili kuleta haki, uhuru na usalama kwa wananchi wa Palestina.

Wazungumzaji katika mkutano huo ni pamoja na Mbunge wa People Before Profit, Richard Boyd Barrett, ambaye alitoa wito wa kufukuzwa kwa Balozi wa Israel, mwanaharakati wa vyama vya wafanyakazi Mags O’Brien na diwani wa Sinn, Féin Daithí Doolan.

Mbunge Barrett ambaye alihutubia mkutano huo, alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuishinikiza Israel kusitisha uchokozi wake dhidi ya Gaza, kwani inawakilisha uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Amesisitiza kuwa, masimulizi ya Israel ni ya udanganyifu na upotoshaji, huku vyombo vya habari vya Magharibi mara nyingi vikionekana kushiriki katika kujaribu kuhalalisha mauaji ya raia wasio na hatia wa Palestina.

Mikutano mingine ya mshikamano wa Palestina pia imefanyika Oktoba 14,2023 katika miji ya Ennis, Cork, Carlow, Limerick na Galway. (WAFA)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news