Maelfu ya watu waandamana nchini Uswizi kupinga uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza

BERN-Maelfu ya wanaharakati, wawakilishi wa mashirika ya kiraia na wanachama wa jumuiya za Waarabu na Waislamu waliingia mitaani Oktoba 14, 2023 katika mji mkuu wa Uswizi wa Bern, wakitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uvamizi wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo pia maandamano yalifanyika jijini Geneva mbele ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, katika kuonesha mshikamano na watu wa Palestina na sababu ya wao kupata haki.

Waandamanaji hao wameitaka Serikali ya Uswizi na jumuiya ya kimataifa kuishinikiza kwa haraka Israel kusitisha mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina wakiwemo watoto.

Vile vile, waandamanaji hao walitaka kuondolewa kwa vizuizi vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza na Israel iwajibike kwa uhalifu wake unaoendelea katika miongo kadhaa iliyopita.(AFP/WAFA/DIRAMAKINI)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news