Makamu wa Rais atembelea Banda la Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Njombe

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Philip Isdori Mpango ametembelea Banda la Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Njombe wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Nne ya Sido yanayoadhimishwa kitaifa mkoa wa Njombe.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda (kulia) alipotembelea Banda la Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Njombe wakati wa kufunga Maonesho ya Nne ya Sido Kitaifa kwenye Viwanja vya Sabasaba tarehe 28 Oktoba 2023tarehe 28 Oktoba 2023.

Dkt,Mpango alitembelea Banda hilo tarehe 28 Oktoba 2023 alipokwenda kufunga Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 23 Oktoba 2023 katika viwanja vya Sabasaba mkoani Njombe.

Akiwa katika Banda la Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Njombe, Makamu wa Rais alielezwa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda namna wizara ya Ardhi inavyotekeleza majukumu kwenye mkoa wa Njombe ikiwemo zoezi la umilikishaji ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda (Kushoto) akisisitiza jambo mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango aipotembelea Banda la Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Njombe tarehe 28 Oktoba 2023.

"Ofisi yetu ya Kamisha hapa Njombe imekuwa ilifanya kazi kubwa ikiwemo kuandaa hati miliki za ardhi na hapa kuna takriban hati 167 ambazo wamiliki wake hawajakuja kuzichukua," alisema Mhe. Pinda.

Akielezea ushiriki wa ofisi yake katika maonesho hayo, Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Njombe Fulgence Kanuti amesema, tangu kuanza kwa maonesho hayo Oktoba 23, 2023 ofisi yake imeweza kuandaa hati milki za papo hapo 18 na wahusika wameweza kuzichukua.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Njombe Fulgence Kanuti (wa tatu kulia) akifuatilia uandaaji hati miliki za ardhi wakati wa Maonesho ya Nne ya Sido Kitaifa kwenye viwanja vya Sabasaba Njombe tarehe 28 Oktoba 2023.

Hata hivyo, amesema hati 167 ambazo wamiliki wake hawajazichukua ni za halmashauri ya Mji wa Njombe na ofisi yake inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wamiliki hao wanazichukua.

"Muitikio wa uchukuaji hati milki za ardhi hapa Njombe siyo mzuri sana, sababu naweza kusema watu hapa wako busy ila wanakuja kuchukua pale panapokuwa na uhitaji maalum kama vile mtu akihitaji mkopo benki,"alisema Kanuti.

Hata hivyo, alisema baadhi ya juhudi zinazofanywa na ofisi yake katika kuhakikisha wananchi wa Njombe wanachukua hati ni kutoa matangazo ikiwemo kutumia redio jamii kuhamasisha.
Huduma zikiendelea kutolewa katika Banda la Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Njombe wakati wa Maonesho ya Nne ya Sido Kitaifa katika viwanja vya Sabasaba Njombe (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Pia Kanuti alisema, Ofisi yake inaendelea na clinic za ardhi katika maeneo mbalimbali ambapo ameweka wazi kuwa mpaka sasa wametembelea baadhi ya mitaa na kuitaja mitaa ya Mgendela, Kihesa, Ramadhani na Kambarage kuwa ni baadhi ya maeneo yaliyotembelewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news