GAZA-Hospitali moja huko Gaza imekuwa ikitumia malori ya ice cream kutoka katika viwanda vya ndani kama vyumba vya kuhifadhia maiti ili kuongeza vyumba vya kuhifadhia maiti vya hospitali vilivyofurika.
Picha na IFP.
Yasser Khatab ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya uchunguzi katika Hospitali ya Martyrs ya al-Aqsa amesema kupitia ujumbe wa video uliotumwa kwa CNN leo Jumamosi kwamba, Hospitali ya Martyrs huko Deir al Balah haiwezi kushughulikia idadi inayoongezeka ya waliokufa.
Vile vile, Khatab aliongeza kuwa baadhi ya miili husalia kuhifadhiwa kwa siku kadhaa kabla ya kukusanywa.
Akitoa ombi la usaidizi, mwanapatholojia wa uchunguzi alisisitiza kwamba Gaza ipo katika mgogoro ambao una madhara hasi kwa raia.
"Gaza inahitaji misaada," Khatab alisema, akibainisha hitaji la friji za kuhifadhia maiti na vifaa vya matibabu pamoja na majeneza na vifaa vya kushughulikia maiti.