MFUMO WA KIELETRONIKI WA USAJILI NA USIMAMIZI WA VIKUNDI VYA KIJAMII VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA NA WAHAMASISHAJI WA BIASHARA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania inapenda kufahamisha Umma kwamba kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imefanya maboresho kwenye mfumo wa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya halmashauri (TPLMIS) kwa kuongeza moduli za usajili na usimamizi wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha (Community Microfinance Groups) na Wahamasishaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha (Microfinance Business Promoters).

Mfumo huu ulioboreshwa wa kielektroniki unalenga kuwezesha vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha na wahamasishaji wa biashara ya huduma ndogo za fedha kuwasilisha maombi ya
usajili na taarifa za uendeshaji kwa njia ya kielektroniki kupitia tovuti https://www.mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz.

Mwongozo wa kuwasilisha maombi ya usajili na taarifa za uendeshaji wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha na wahamasishaji wa biashara ya huduma
ndogo za fedha kupitia mfumo wa kieletroniki pamoja na fomu zinazohusu maombi ya usajili vimewekwa kwenye tovuti ya mfumo huu kwa ajili ya rejea kwa watumiaji.

Hivyo, vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha na wahamasishaji wa
biashara ya huduma ndogo za fedha wanashauriwa kuendelea kuwasilisha maombi ya usajili na taarifa za uendeshaji katika halmashauri husika kupitia mfumo huu mpya ili yaweze kufanyiwa kazi na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 23 Oktoba 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news