ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 umepitiliza ahadi kwa kuvuka lengo kwa miradi ya maendeleo ya huduma za jamii liyopangwa kutekelezwa ikiwemo sekta ya elimu.
Ni kwa kujengwa kwa skuli za kisasa za msingi na sekondari za ghorofa, sekta ya afya kukalimika kwa hospitali za wilaya na kujenga hospitali za mikoa, miradi ya maji, ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa wanananchi.
Sambamba na ujenzi wa barabara za mijini na vijijini, ujenzi wa bandari, ongezeko la mishahara ya wafanyakazi pamoja na ongezeko la pensheni kwa wastaafu na jamii.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Mkoa wa Mjini Magharibi waki akiweka jiwe la msingi mradi wa nyumba za ZSSF Tomondo viwanja vya Magereza.
Pia, mradi wa nyumba za gharama nafuu za Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) Mji wa Dkt.Hussein Mwinyi Mombasa kwa Mchina Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.
Vile vile, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameweka jiwe la msingi Skuli ya Sekondari ya Mtopepo Wilaya ya Magharibi A na jiwe la msingi Skuli ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.