MIAKA MITATU YA RAIS DKT.MWINYI: Vijana wa masumbwi wamepata ajira za uhakika

ZANZIBAR-Moja ya Mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka Mitatu ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi ni kurejesha mchezo wa ngumi za kulipwa ambao ulipigwa marufuku Zanzibar kwa zaidi ya miaka 50.

Uamuzi wa Rais Dkt.Mwinyi kuruhusu mchezo wa ngumi za kulipwa ni kufungua fursa za ajira kwa vijana pamoja na kutangaza utalii wa Zanzibar.

“Sina budi kumshukuru Rais Dk.Mwinyi kwa kurejesha Ndondi, tumepata ajira za uhakika ambapo hapo awali tulikuwa tunacheza kwa kujificha,” amesema Miraji Iddi Juma (38) mkaazi Kianga, Unguja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news