ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ametekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020 kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuwatengenezea mazingira mazuri rasmi ya kuyafanyia biashara zao ikiwemo mama nitilie, mafundi gereji, wafua vyuma, wauza mbao na wengineo.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa halmashauri kuweka viwango vya kodi kwa wajasiriamali vinavyohimilika na siyo kuweka kodi za bei ya juu.
Vilevile ameagiza wafanyabiashara na wajasiriamali watakaoanza kufanya biashara kituo hicho wasilipe kodi kwa miezi mitatu bure walipe kuanzia Aprili mwaka 2024.