KIGOMA-Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor H.Seff amekutana na watumishi wa TARURA Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo amepokea taarifa mbalimbali za kiutendaji na kuwataka kuzingatia uadilifu na kutimiza wajibu.

"Nimepata nafasi ya kumsikiliza kila mmoja wenu na changamoto zilizo ainishwa zitafanyiwa kazi, wito wangu kwenu ni kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake kwa wakati na kwa uadilifu ili tuweze kufikia malengo kwa kutoa huduma bora ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi,"amesema Mhandisi Seff.