Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Mativila aipongeza TARURA

DODOMA-Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kazi wanazoendelea kufanya katika maeneo mbalimbali nchini.
Mhandisi Mativila ametoa pongezi hizo wakati alipokutana na kufanya kikao na Menejimenti ya Wakala huo kwenye ukumbi wa TARURA uliopo mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma.
Mhandisi Mativila ameitaka Menejimenti hiyo kusimamia kazi kwa weledi na kuhakikisha kazi zote zinakamilika kwa wakati.

Aidha, amesisitiza matumizi ya teknolojia mbadala kwenye ujenzi wa madaraja ya mawe kwa lengo la kufikisha huduma kwa wananchi na kwa gharama nafuu.
TARURA inaendelea na kazi ya ujenzi,ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za wilaya zenye urefu wa Kilomita 144,429.77 nchi nzima lengo ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma za kijamii na kuweza kusafirisha mazao na bidhaa zao kirahisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news