Operesheni ya DCEA yarejea tena Arumeru, magunia 237 ya bangi yateketezwa

ARUSHA-Kufuatia operesheni maalumu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) iliyofanyika wilayani Arumeru mkoani Arusha wamefanikiwa kukamata magunia 237 ya bangi na mbegu zilizosafishwa tayari kwa kupandwa kilogramu 310 ambazo zimeteketezwa.
Akizungumza wakati wa uchomaji wa bangi hizo wilayani humo, Innocent Masangura ambaye ni Mkuu wa Operesheni wa mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini kwa niaba ya Kamishina wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Aretas James Lyimo ametoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kuachana na kilimo hicho kwa kuwa msako bado unaendelea.
"Tumefanya operesheni hii kutokana na kukithiri kwa kilimo cha bangi katika Wilaya ya Arumeru. hivyo tumeamua kufanya iwe ni operesheni maalumu na itakuwa ni operesheni ya mara kwa mara.

"Wito wangu kwa wakazi wa Wilaya ya Arumeru ambao wanajihusisha na kilimo cha bangi, hizi operesheni tutaendelea kuzifanya kama tulivyofanya hii, kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya ya Arumeru.
"Biashara ya bangi haifai, biashara ya bangi itawatia matatizoni kutokana na moto tulioanza nao utakuwa ni endelevu na kama alivyosisitiza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwamba bangi na dawa zote za kulevya zipotee katika uso wa Tanzania.
"Hivyo, tutalitilia hilo mkazo, sisi Kanda ya Kaskazini tumeanza na huu ni mwanzo tu, tutakuwa na mwendelezo wa mara kwa mara tukishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya wilaya husika na pia kwa kuzunguka mikoa yote ambayo sisi tunaisimamia ambayo ni Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara,"amefafanua Masangura kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa DCEA,Aretas James Lyimo.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Sara Ndaba amesema;
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Emmanuela Kaganda amesema kutokana na oparesheni walizozifanya wahusika wamebadili mbinu hivi sawa wanazificha nyumbani na kwenye makorongo na si mashambani kama ilivyokuwa hapo awali.

Aidha ameongezea kuwa kwa sasa wanaendelea na utafiti wa kupata zao mbadala yatakayo stawi eneo hilo ikiwa ni jitihada za kufanya wananchi hao waache kilimo hicho.
"Tumeendelea na zoezi la kupamabana na dawa za kulevya, na kwa wilaya hii mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni ajenda ya kudumu.

"Na kila mwezi tumekuwa tukifanya mazoezi haya, ya kwenda kusaka dawa za kulevya aina za bangi, kwenye maeneo ambayo zao hili linalimwa, kwa mwezi Septemba Wilaya ya Arumeru, Kamati ya Usalama tukishirikiana na Ofisi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ambao kwa sasa wana ofisi zao Mkoa wa Arusha tulifanikiwa kukusanya gunia 90 za bangi.

"Na kwa mwezi huu Oktoba tumeweza kukusanya gunia za bangi 225. Na kufanya jumla ya gunia za bangi ambazo zimekusanywa ndani ya miezi miwili, mwezi wa Septemba pamoja na mwezi huu wa Oktoba kuwa gunia 316.
"Na, siku ya leo tunateketeza gunia 237 za mmea aina ya bangi, lakini gunia nyingine zilizobaki kwa sababu ya changamoto ya usafiri tuliziteketeza kwenye eneo la tukio.

"Sambamba na hilo tunateketeza mbegu za mmea huu wa bangi kilo 310 na hizi bangi ambazo tunazichoma sasa hivi, sasa hivi hatuzipati tena mashambani bali mwanzo tulikuwa tunakuta wamezitunza majumbani, zipo kwenye magunia tayari kwa ajili ya kuziuza.
"Lakini, sasa hivi baada ya kufanya operesheni za huko nyuma, sasa hivi wametoa majumbani wanazificha kwenye makorongo na wakishavuna mahindi wanaweka chini ya yale mabua ya mahindi kwa ajili ya kuhakikisha wanalificha hili zao kwa ajili ya kulipeleka sokoni.

"Kwa hiyo, tumeendelea kupambana nao na tumeendelea kubaini hizo mbinu zote ambazo zinatumika katika kuficha mmea huu ambao ni haramu na unaharibu sana kizazi na vijana wetu wa Kitanzania.
"Serikali ya wilaya kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na wizara nyingine, tumeendelea kutafuta njia mbadala au kutafuta mazao mengine mbadala kwa ajili ya kulimwa kwenye maeneo haya, kwa sasa tupo kwenye mazungumzo na makampuni ambayo yananunua pareto na wengine wameshafika ofisini,

"Na wataalamu wetu wa kilimo wameshakutana nao, nami ninategemea kukutana nao ndani ya wiki hii kwa ajili ya kuweka mpango wa kwenda kuanza kufanya uhamasishaji kuweza kulima kilimo cha pareto.

"Lakini pia kupitia Wizara ya Kilimo tunaendelea kushirikiana nao na wataalamu wetu wanaendelea kufanya utafiti wa mazao mengine ambayo yana high value kwa ajili ya kwa ajili ya kuwa zao mbadala la zao hili la bangi."

Uongozi wa eneo hilo pamoja na Wananchi wamepongeza zoezi hilo kwa kueleza jinsi vijana walivyoathirika na matumizi ya bangi ikiwemo suala la momonyoko wa maadili. Chini wasikilize Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kikatiti, Raphael Nnko na wananchi akiwemo Bayo Mashaka;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news