Prof.Muhongo abisha hodi kila kata kupeleka miundombinu ya elimu

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Vijijini wanaendelea na ziara za uchangiaji na uhamasishaji wa ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye sekondari jimboni humo.

Hayo yameelezwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo la Musoma Vijijni Oktoba 4, 2023.

Taarifa hiyo imebainisha kwamba Jumatatu ya Oktoba 9,2023 majira ya Saa 4 asubuhi itakuwa Mtiro Sekondari iliyopo katika Kata ya Bukumi. Na Saa 8 mchana itakuwa Nyanja Sekondari katika Kata ya Bwasi.

Aidha, wananchi watapata muda wa kutosha kuwasilisha, kwa Mbunge wao, kero na matatizo yanayowakabili kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Huku wananchi na wadau mbalimbali wakiombwa kuhudhuria.

Wananchi wa Musoma Vijijini wakizungumza na DIRAMAKINI wamepongeza juhudi kubwa za maendeleo zinazofanywa na Mbunge huyo katika sekta zote akishirikiana na Serikali kwa karibu pamoja na wananchi sambamba na kusikiliza kero zao na kuzipatia utatuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news