Prof.Oreku atoboa siri kuhusu mifumo ya elimu huria, masafa na mtandao

PWANI-Mifumo ya Elimu Huria, masafa na mtandao ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha elimu bora na ya gharama nafuu inawafikia wananchi wote popote pale walipo wakiwa wanaendelea na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kutoa huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Prof. George Oreku wakati akifunga Kongamano la Kimataifa la kwanza na tafakuri ya mifumo ya elimu kwa maendeleo endelevu lililofanyika mjini Kibaha mkoani Pwani katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Septemba 27 hadi 29, 2023. 

Prof. Oreku alisema, "Mifumo ya elimu hasa katika kipindi hiki cha ongezeko kubwa la mahitaji ya wanafunzi wengi kujiunga na elimu inahitaji kutafitiwa vya kutosha ili kuimarishwa zaidi. 

"Mifumo ya elimu huria, masafa na mtandao inaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kupokea wanafunzi wengi kwa wakati mmoja kuliko mifumo mingine.

"Uwekezaji katika mifumo hii utasaidia sana kuipeleka elimu kwa watu wote wakiwa popote pale mijini na vijijini wakiendelea na shughuli zao za uzalishaji mali. 

"Kubwa zaidi ni kwamba, mifumo hii humwezesha mwanafunzi kujifunza na kutumia ujuzi alioupata papo kwa papo jambo ambalo litaleta maendeleo endelevu katika jamii,"amesema.

Prof. Oreku aliendelea kueleza kwamba, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ni taasisi ya elimu ya juu ambayo ni mtekelezaji mkuu wa kutoa elimu kwa kutumia mifumo hiyo na kutoa wahitimu wenye ujuzi, maarifa na weledi wa hali ya juu katika fani mbalimbali.

Prof. Oreku ambaye alifunga kongamano hili kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Elifas Bisanda, aliwashukuru washiriki wote kwa ushiriki wao wengine wakitokea nje ya nchi ambapo mataifa zaidi ya 14 yameshiriki kwa mafanikio makubwa sana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news