Rais Abbas afanya mazungumzo kwa simu na Rais Lula da Silva kuhusu vita Gaza

RAMALLAH-Rais Mahmoud Abbas wa Palestina jioni ya Oktoba 14, 2023 amejadili kuhusu changamoto za hivi karibuni na maendeleo huko Palestina kwa njia ya simu na mwenzake wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva.

Kupitia majadiliano hayo,Rais Abbas alisisitiza udharura wa kusitisha uchokozi wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na kuhakikisha ulinzi wao unaheshimiwa.

Pia alitoa wito wa kufunguliwa mara moja kwa njia za kibinadamu huko Gaza, utoaji wa vifaa vya matibabu, na usambazaji wa vifaa muhimu, ikiwa ni pamoja na maji, umeme, na mafuta kwa wakazi wa Gaza.

Rais alikataa kufukuzwa kwa watu wa Gaza, akisisitiza kwamba kitendo kama hicho kitakuwa janga lingine kwa watu wake huko Gaza.

Alisisitiza dhamira yake ya kulinda raia wa pande zote mbili na kutoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kiraia na mateka, akisisitiza kukataa kwake ghasia na kujitolea kwa jumuiya ya kimataifa katika kutekeleza kwa vitendo mikataba iliyotiwa saini.

Rais Abbas pia alisisitiza kujitolea kwake kutafuta suluhu ya kudumu kwa njia ya kufikia malengo ya kitaifa na kukomesha uvamizi wa Israel.

Pia, Rais alitoa shukurani zake kwa Rais Lula da Silva kwa msimamo wake wa kuunga mkono na kujitolea kwa kadhia ya Palestina, hasa kupatikana kwa taifa huru la Palestina na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wake.

Wakati huo huo, Rais Abbas aliipongeza Brazil kwa jukumu lake la kuwajibika na la kufuata sheria katika majukwaa ya kimataifa.

Kwa upande wa Brazil, Rais Lula da Silva alithibitisha mshikamano wake na wa watu wa Brazil kwa watu wa Palestina katika kutafuta haki zao halali hususani uhuru na haki ya kudumu.

Amesisitiza haja ya kutoa msaada wa kimatibabu na kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza na kutoa wito wa kuwepo kwa amani na usalama katika eneo hilo. (WAFA/DIRAMAKINI)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news