Rais Abbas apokea simu kutoka kwa Rais Biden kuhusu vita Gaza

RAMALLAH-Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas amethibitisha jioni ya Oktoba 14, 2023 kufanya mazungumzo ya simu na Rais wa Marekani, Joe Biden.

Wawili hao wamejadiliana kuwa,amani na usalama katika eneo hilo vitapatikana tu kupitia utekelezaji wa suluhu ya mataifa mawili yenye msingi wa Kimataifa na maazimio yenye uhalali.

Ili kufikia lengo hilo, Rais alisisitiza haja ya kusimamisha mashambulizi yote na kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu kuhusu kile kinachoendelea katika Ukanda wa Gaza.

Wakati wa mazungumzo ya simu na Rais wa Marekani, Rais Abbas alisisitiza ulazima wa kuruhusu njia za dharura za kibinadamu kufunguliwa katika Ukanda wa Gaza.

Sambamba na kutoa vifaa vya msingi na vifaa vya matibabu, kupeleka maji, umeme na mafuta kwa wananchi wa huko. Pia, alikataa kabisa kufukuzwa kwa Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo, Rais Abbas alitaka kukomeshwa mara moja kwa mashambulizi ya Walowezi wa Israel dhidi ya watu wake katika miji ya Palestina, vijiji na kambi za wakimbizi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kukomeshwa kwa uvamizi wa magaidi hao wenye itikadi kali katika Msikiti wa Al-Aqsa, ambao unasababisha kuongezeka kwa hali hiyo.

Rais Abbas pia alithibitisha kukataa kwake mazoea yanayohusiana na kuua au kuwadhulumu raia wa pande zote mbili, akitoa wito wa kuachiliwa kwa raia, wafungwa na mateka.

Vile vile, Rais huyo alikataa ghasia akitaka kufuatwa njia halali za kupata usuluhiso kupitia mkondo wa Kimataifa ili wananchi waendelee kuishi kwa amani.

Rais Abbas alimshukuru Rais Biden kwa mwelekeo wake na juhudi za utawala wake kufikia usalama, utulivu na amani katika eneo hilo.

Amesisitiza utaya wa upande wa Palestina wa kujishughulisha na kufikia amani ya haki katika eneo lao haraka iwezekanavyo na kusisitiza kwamba usalama na amani vitapatikana tu kwa kuwapa wananchi wa Palestina haki zao kamili za kisheria.

Rais alisisitiza umuhimu wa kuunda suluhu ya kisiasa na kutekeleza suluhisho la serikali mbili kwa kuzingatia uhalali wa kimataifa,uhuru wa watu wao katika nchi yao huru na Jerusalem Mashariki ukiwa mji mkuu wake kwenye mipaka ya 1967.(WAFA/DIRAMAKINI)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news