Rais Abbas, Waziri Mkuu wa Uholanzi wajadiliana kwa simu vita Gaza

RAMALLAH-Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amepigiwa simu jioni ya Oktoba 14,2023 na Waziri Mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte.

Wawili hao wamejadili changamoto zinazoendelea Palestina na namna ya kutafuta njia za kusitisha mara moja uchokozi wa Israel dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza.

Wakati huo huo, Rais Abbas amesisitiza umuhimu wa kutoa ulinzi kwa wakazi wa Palestina, akitoa wito wa kufunguliwa kwa haraka njia za kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

Amesisitiza umuhimu wa kuwasilisha vifaa muhimu, vifaa vya matibabu, pamoja na kuhakikisha utoaji wa maji, umeme, na mafuta kwa wakazi wa Palestina wa Gaza.

Rais Abbas ametoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu wa Uholanzi kwa msaada ambao tayari umetolewa na nchi yake na misaada ya kibinadamu inayotolewa katika nyakati hizi ngumu.

Amezitaka pande zote husika kutoa shinikizo kwa Israel kuwazuia Walowezi wenye itikadi kali kuacha kushambulia miji ya Palestina, vijiji na kambi za wakimbizi, akitaka hatua zichukuliwe kuzuia watu wenye msimamo mkali kuvamia maeneo matakatifu ya Kikristo na Kiislamu mjini Jerusalem.

Rais amekataa kuhamishwa kwa watu wa Palestina kutoka Ukanda wa Gaza, akisisitiza kwamba hatua hiyo itakuwa janga ambalo Wapalestina hawataliruhusu kamwe.

Rais Abbas alisisitiza kuwa, usalama na amani vinaweza kupatikana kwa kuwapa watu wa Palestina haki zao halali kwa kutafuta suluhu ya kisiasa na kutekeleza suluhisho la mataifa mawili kwa kuzingatia uhalali wa kimataifa.(WAFA/DIRAMAKINI)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news