Rais wa IPU ataka Watanzania washirikiane ili kuionesha Dunia utofauti

DODOMA-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson ameomba ushirikiano kutoka kwa Watanzania wote ili kuionyesha Dunia utofauti wa Tanzania kuishika nafasi hiyo.

Dkt. Tulia ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania ametoa kauli hiyo leo Bungeni Dodoma katika halfa ya kumpokea akitokea Nchini Angola ambako alishinda nafasi ya Rais wa IPU katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27, 2023.

Amesema Tanzania inayo nafasi ya kufanya vizuri katika nafasi hiyo iwapo kutakuwepo ushirikiano kutoka kwa watu wote.

“Nafasi hii ni yetu wote, ukiwa na ushauri wa namna ya kuupeleka umoja huu mbele tuletee ili tufanye vizuri, usisuburi tushindwe.

“Ifike mahali tukitaka nafasi nyingine kimataifa tupate kwa kuwa tulifanya vizuri kwenye hii, tutasikiliza ushauri wenu, ninaamini tutafanya vizuri na Dunia itajua kwamba tulishawahi kushika hii nafasi, viongozi wa dini muendelee kutuombea,” alisema.

Alitoa wito kwa Watanzania kuondoa tofauti zao kwenye masuala ya uwakilishi wa Tanzania Kimataifa kwa kuacha kuidharau nchi mbele ya nchi nyingine.

“Nafasi kama hizi siyo za kuzipiga teke, tujitahidi kujizuia hasa katika mambo ya kimataifa, tusifike mahali ya kuiuza au kuidharau nchi yetu kwa wengine, usiungane na adui kwa ajili ya kulipiga Taifa lako,” alisema.

Mheshimiwa Dkt. Tulia alitoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kumuwesha kupita katika mchakato wa uchaguzi uliodumu kwa miezi mingi na kwamba isingiwezekana bila yeye kutoa kibali.

“Vilevile namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Hasan Suluhu kwa kuridhia nigombee nafasi hii, nafasi kama hii huwezi kugombea bila nchi yako kuruhusu na anayeruhusu ni Mheshimiwa Rais.

Awali Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa akitoa salamu za Serikali alisema Mheshimiwa Rais Samia Hasan Suluhu, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango wanampongeza kwa ushindi mnono wa nafasi hiyo nyeti.

“Sisi tumefarijika kama Serikali kwa sababu moja kati ya majukumu yako utakuwa unashiriki vikao vyote vya Umoja wa Mataifa, tunayo mikataba mingi katika nyanja za kimataifa, tutakutumia wewe kuingiza".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news