Salamu za Kumbukizi ya Miaka 24 ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka kwa wadau mbalimbali nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu wakati wa Misa Maalum ya Kumbukizi ya kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika Babati mkoani Manyara leo Oktoba 14, 2023.