NA FRESHA KINASA
WADAU mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wazawa wa Kijiji cha Nyambono Kata ya Nyambono na Kijiji cha Kaburabura Kata ya Bugoji katika Wilaya ya Musoma mkoani Mara wameombwa kujitokeza kuchangia ujenzi wa zahanati mpya zinazojengwa katika vijiji vyao.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika kuhakikisha zanahati hizo mpya zinajengwa katika vijiji hivyo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof.Sospeter Muhongo ataambatana na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) ya Musoma Vijijini kuchangia na kuhamasisha ujenzi wa zahanati mpya za vijiji hivyo.
Kwa mujibu taarifa hiyo Alhamisi ya Oktoba 12, 2023 majira ya saa 4 asubuhi itakuwa katika Kijiji cha Nyambono kilichopo Kata Nyambono na siku hiyo hiyo majira ya saa 9 alasiri itakuwa katika Kijiji cha Kaburabura Kata ya Bugoji.
"Wadau wetu wa maendeleo wakiwemo wazaliwa wa vijiji/kata hizo wanaombwa kuchangia miradi hiyo ya ujenzi wa zahanati za vijiji hivyo. Karibuni Sana kwenye harambee za maendeleo ya Vijijini mwetu." imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.