Serikali yaahidi maboresho zaidi Sekta ya Michezo

MOROGORO-Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema Serikali itaendelea kuweka mkazo kwenye michezo ya aina zote katika ngazi zote kwa kuwa michezo ni ajira, biashara na uchumi.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Oktoba 29 2023 wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati akifunga mashindano ya Gofu ya Kilombero Open yaliyoambatana na ugawaji wa zawadi kwa washindi.

"Sisi wasaidizi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kazi yetu ni kutekeleza kwa vitendo maono yake na moja ya shughuli tulizopewa ni kuhakikisha mkazo unawekwa sio kwenye mchezo mmoja lakini kwenye michezo yote na kwenye ngazi zote mpaka chini, jana nilifunga ligi kwenye kata inaitwa Mwaya kule Ulanga, unaweza kuona nimeenda kwenye mashindano ya jimbo ya mpira wa miguu na Netiboli na leo niko hapa, yote ni kutekeleza maono ya Mhe. Rais ya kwamba tuweke mkazo na tuhakikishe kwamba kila mchezo kwenye ngazi yoyote jicho la Serikali linakuwepo," amesisitiza Mhe. Mwinjuma

Mhe. Mwinjuma amekiomba kiwanda cha Sukari kilombero licha ya kuwekeza kwenye mpira wa gofu kiwekeze pia kwenye mpira wa miguu kwa kuwa na timu ya Mpira wa miguu ili vijana waendelee kunufaika na Michezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news