Tanzania kinara utekelezaji wa afua za kujiandaa na kudhibiti magonjwa kupitia mtandao

LIVINGSTONE-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imeibuka mshindi wa tuzo ya ufanisi katika utekelezaji wa mradi wa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kusimamiwa na taasisi ya ECSA- HC kwa kuwa na mfumo bora wa mafunzo kwa njia ya mtandao (eLearning) ambao umekuwa msaada kwa wataalamu wengi.
Tanzania imefikia hatua hiyo wakati ilipohudhuria mkutano wa nchi zinazotekeleza mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kusimamiwa na taasisi ya ECSA- HC uliofanyika katika mji wa Livingstone nchini Zambia kuanzia tarehe 17 hadi 18 Oktoba 2023.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Dkt. Saitore LaizerMkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt John Jingu.

Dkt. Saitore amesema kupitia jukwaa hilo Tanzania imepata fursa ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa afua za mradi wa kujiandaa na kudhibiti magonjwa na majanga yanayoathiri afya na vile vile jinsi ya kuendeleza uwezo ambao umekwishajengwa.

Dkt. Laizer ameongeza kuwa kwa kushirikiana na wataalamu wengine kutoka Wizara hiyo waliombatana nao, wamekuwa na mikutano ya pembeni na wadau wa Mbalimbali maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia ili kupata uwezekano wa kuwa na mradi mwingine wa kuendeleza afua nyingine zaidi. Baadhi ya Nchi zilizoshiriki mkutano huo ni Lesotho, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Tanzania na wenyeji Zambia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news