IRINGA-Timu ya mpira wa miguu ya TARURA imejinyakulia pointi 3 dhidi ya timu ya RAS Kilimanjaro wakati wa mchezo wa makundi katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa.

Ushindi huo umetokana na timu ya RAS Kilimanjaro kufika uwanjani na wachezaji pungufu (4) ikiwa ni kinyume na kanuni ya mpira wa miguu na hivyo kusababisha mchezo huo kushindwa kuchezwa.

Kutokana na hali hiyo mwamuzi wa mchezo huo alimaliza mchezo na kuipa timu ya TARURA ushindi wa pointi 3 na magoli matatu.

Katika kundi (H) TARURA inaendelea kuongoza kwa pointi 12 katika mechi zake nne walizocheza na hivyo kubakiwa na mchezo mmoja utakaochezwa hapo kesho dhidi ya SHERIA.


Kundi (H) linaundwa na timu za Elimu, Ardhi, RAS Kilimanjaro, Sheria, Wakili Mkuu pamoja na TARURA.