TARURA Morogoro: Sisi hatulali,kila mmoja azingatie ubora wa kazi

MOROGORO-Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmauel Ndyamkama amesema kuwa ataendelea kusimamia ubora wa kazi zinazofanyika katika Mkoa huo kwa kuzingatia matakwa ya mikataba inayosainiwa baina ya TARURA na Makandarasi.

Hayo yamejiri wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la Ruhembe liliopo Kata ya Ruhembe Jimbo la Mikumi katika Wilaya ya Kilosa .

Mhandisi Ndyamkama ameeleza kuwa daraja hilo lenye urefu wa mita 40 limefikia asilimia 80 ya ujenzi wake na kwamba hatua zote zinaendelea kufuatwa kulingana na mkataba ili likamilike na kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

"Daraja hili kama linavyoonekana ni sehemu ya miradi inayotekelezwa katika mkoa huu, kuna baadhi ya watu wasio na nia njema wanaojaribu kupotosha juu ya jitihada hizi lakini kimsingi kazi hizi zinajionesha na ubora unazingatiwa,"amesema mhandisi Ndyamkama.

“TARURA Morogoro haitosita kuwachukulia hatua makandarasi na hata watumishi watakaobainika kuzorotesha ama kuhujumu kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara na kwamba atahakikisha lengo la Serikali la kutoa huduma bora kwa wananchi linafikiwa”Aliongeza

Kwa upande wake Bw. Hassan Salum Mwaking'inda mkazi wa Kata ya Ruhembe amesema kuwa ujenzi wa Daraja hilo utasaidia wananchi katika kuzifikia huduma za kijamii pamoja na kufanya biashara.

"Daraja hili ni mkombozi wetu maana likikamilika litatusaidia kijamii na kiuchumi hasa katika kusafirisha miwa kwenda kiwandani,"amesema Salum.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news