LINDI-Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Lindi inaendelea na kazi ya kuunganisha na kufungua barabara katika maeneo mbalimbali ili kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Liwale, Mhandisi Livingstone Shija amesema kuwa malengo ya TARURA katika Wilaya hiyo ni kuhakikisha wananchi wanasafiri kwa urahisi ili kuzifikia huduma za kijamii na kiuchumi.
Katika kuhakikisha hilo, TARURA imefanya matengenezo ya Barabara ya Liwale-Lilombe - Mbwemkuru yenye urefu wa Kilomita 83 ambapo kati ya hizo kilomita 20 zimefunguliwa.

