DAR ES SAALAM-Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesema limepokea kwa furaha uteuzi wa ndugu Mobhare Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Pia linampongeza kwa uteuzi huo wa Oktoba 1, 2023. TEF imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uteuzi wa mtu sahihi kushika wadhifa huo;